Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 959 registered users
The newest registered user is Mfaume.Bodde

Our users have posted a total of 1232 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 3 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 3 Guests :: 1 Bot

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

Naomba ufafanuzi wa namna ya kusitisha zabuni

Go down

Re: Naomba ufafanuzi wa namna ya kusitisha zabuni

Post  RSM on Wed Aug 28, 2013 4:28 pm

Id2013 na Raporini,

Mmeleta mada ambayo inajumuisha changamoto nyingi walizonazo wenzetu wa Halmashauri za Serikali za Mitaa.

Id2013 umechambua vizuri hoja alizozitoa Raporini. Ila  Kanuni za Kuunda Bodi za Zabuni za Serkali za Mitaa za Mwaka 2007 zimetoa majukumu kwa Kamati ya Fedha ya Halmashauri kuhusiana na masuala ya zabuni lakini sio katika mchakato wa zabuni. Majukumu yao yanajumuisha kuidhinisha Bodi ya Zabuni iliyoundwa na Mkurugenzi, kuidhinisha Mpango wa Manunuzi wa Mwaka, kupitia ripoti ya robo mwaka ya Utekelezaji wa Mpango wa ununuzi.

RSM

Posts : 150
Join date : 2009-08-11

View user profile

Back to top Go down

Re: Naomba ufafanuzi wa namna ya kusitisha zabuni

Post  id2013 on Tue Aug 27, 2013 5:39 pm

Raporini,
Karibu sana kwenye jukwaa la kitaalamu. Binafsi nitajaribu kujibu au kukupa ushauri wa jumla kulingana na ulivyoleta mada yako. Kwanza kabisa nina imani kwamba zabuni hiyo ilikuwepo kwenye mpango wa ununuzi wa mwaka (APP) kwa mujibu wa Section 45, PPA 2004 na kwamba mpango huo ulipitishwa na menejimenti kabla ya kwenda Bodi ya Zabuni kuidhinishwa na kwamba kabla mpango huo hujaenda menejimenti mahitaji hayo kama wewe mtaalamu uliyatoa kutoka kwenye bajeti nzima ya H/shauri na bajeti na mipango yote kupitishwa na baraza au madiwani hao hao! hilo kama ninakosea utanisahihisha.

Pili, baada ya zoezi zima la kuwa na mpango wa ununuzi na ndio dira ya utekelezaji wa masuala yote ya ununuzi na kwamba uliidhinishwa na Bodi ya Zabuni husika. Kwa kuongezea ni kwamba mchakato wote wa kuanza kutangaza na kutoa nyaraka za zabuni ulipata ridhaa ya Bodi ya zabuni kwa mujibu wa Section 30(c) na Section 31 (a). Bila shaka yote hayo yalitekelezwa.
Kwa kuzingatia hayo mambo mawili niliyoandika hapo juu, nakushauri urudishe Bodi ya zabuni suala hilo ukipeleka mapendekezo yafuatayo;-
Kwanza kubadili methods of procurement kutoka ile iliyoanishwa kwenye APP yako na ndio hiyo uliitumia awali kwenda procurement method nyingine ambayo mnaona itawapa value for money katika utekelezaji wake lakini la kuzingatia ni uwazi na thamanai ya pesa hatimae. Sababu za kubadilisha njia ya ununuzi ni lazima ielezwe bayana kwa Bodi ya zabuni na kwamba itafaidisha vipi halmashuri badala ya kutumia ile ya awali iliyopendekezwa kulingana na Section 43 (c) of PPA 2004.

Kwa kifupi hapa ni Bodi ya zabuni pekee ndio yenye mamlaka ya kusitisha zabuni hiyo na kubadili chochote kinachotakiwa kufanyika kuhusuiana na zabuni husika. Bila ya kufanya hivyo utakuwa umekiuka Sec. 31(a) na Bodi ya zabuni wasipohusishwa watatumia Sec 30 (4). Bodi ya zabuni kwa mujibu wa PPA 2004 na kanuni zake ndio yenye uwezo wa kufanya maamuzi yeyote kuhusiana na zabuni tajwa isipokuwa lazima makubaliano pia yawe yamefikiwa katika baraza na Accounting Officer kabla haijaenda bodi ya zabuni.

Sasa narejea kwenye ishu ulizosema zinahitaji ushauri
1. sheria na kanuni unayohitaji kuhusu kusitisha zabuni inapotokea mkanganyiko ulileta kwenye jukwaa ni sheria iliyochini ya mamlaka na nguvu za bodi ya zabuni kuamua kusitisha au kuendelea na zabuni hiyo provided mivutano ya waali itakuwa imekwisha (Yaani Baraza lieleze bayana na uthibitisho wa kile wanachokidai na kwamba Accounting Officer) akubaliane na ushauri huo vinginevyo sheria na kanuniza PPA 2004 haziitambui Baraza wala mtu mwingine isipokuwa ni Bodi ya Zabuni Sec 31 of PPA 2004.
2.Katika suala hili Raporini unanichanganya, umesema Menejimenti wanasema muda wa zabuni umekwisha?, Je Wewe ni niani hapo?, Je Menejimenti ndio wanafahamu muda wa Zabuni kwisha au lah?, sio hilo ni jukumu la Bodi ya zabuni pamoja na PMU kuratibu mchakato wote wa zabuni na kusihauri Menejimenti?. Je kama muda ulikwisha, una maanaisha zabuni zilishapokelewa na kufanyiwa kazi na kwamba mzabuni teule alishapatikana?
Kama sio hivyo muda ulikwisha na zabuni hazijapokelewa kwa ajili ya mvutano?, kama hili ni sawa ulitakiwa kuwaandikia barua wazabuni kuwaomba ku-extend muda wa kuwasilisha zabuni zao kwa uangalifu ukitumia Regulation 84(3-4)/GN NO.97, 2005 ambayo kwa namna moja au nyingine umeivunja kwa ajili ya kuwa na mivutano hiyo.
Hapa pia kwa wazabuni waliokosa vitabu hivyo haki yao ni kukushitaki kwa kukiuka Regulation ya 53/GN 97, 2005 ambapo ulishindwa kuandaa nyaraka za zabuni za kutosha kwa hiyo kulikuwa na uzembe kwako.

3. Ndio kuna haja ya kuwajulisha wazabuni hao kwa kuwaeleza sababu za kusitishwa zabuni hiyo ambazo labda zipo nje ya uwezo wa PE husika mpaka hapo itakavyoamuliwa vinginevyo na uawatombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Lakini hayo yote Bodi ya zabuni nisharti kuridhia pia kusitishwa kwa zabuni kwa sababu ndio iridhia kutangazwa kwa zabuni hiyo, Accoutning officer yeye ana commuicate tu kwenye public kwamba kasitisha (Cancel) zabuni hiyo.

4.Kwa kifupi Baraza halitambuliwi na PPA 2004 na Kanunzi zake labda ile ya Local Government angalia kama inaruhusu lakini principle legislation ambayo ni PPA 2004, iliyotungwa na Bunge haiwatambui katika mamlaka hiyo.

5.Bodi ya zabuni ikiridhia na kwa sababu nilizotaja awali haina tatizo lolote ila wazabuni huwezi kuwazuia kupeleka malalamiko kwenye vyombo husika kwani ni haki yao kwa mujibu wa Regulation 79/GN 97, 2005 of PPA 2004 baada ya kufahamu jambo lolote kuhusiana na zabuni husika. Na suala la gharama kurudishiwa au la na mambo mengine yataalimuwa kulingana na taratibu zilioelezwa katika kanuni hii.

Napenda kuwasilisha Naporini

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

Naomba ufafanuzi wa namna ya kusitisha zabuni

Post  raporini on Wed Aug 14, 2013 3:36 pm

Kwanza nashukuru kwa kupata fursa ya kujiunga na forum hii. Naomba kupata maelekezo ya namna ya kusitisha zabuni kabla ya kupata maelekezo au ufafanuzi kwanza nieleze hali ilivyo na kile kilichotokea:
Halmashauri ya wilaya imetangaza zabuni ya ukusanyaji wa mapato katika ''lots'' katikati mwezi Juni, 2013 na wazabuni mbalimbali wamejitokeza kushindania zabuni hiyo kiasi kwamba vitabu vya zabuni vilivyoandaliwa vilinunuliwa na kuisha na hivyo wazabuni wengine kukosa. Pili katika baraza la madiwani liliamuru menejimenti ya halmashauri hii kuisitisha mchakato wa ununuzi hadi pale baraza litakapohakikisha kuwa menejimenti inauwezo wa kusimamia mzabuni, kutambua vyanzo vinavyobinafsishwa na kiwango cha ukusanyaji (revenue potential), kwa ufupi ni kama kuna mvutano kati ya baraza na menejimenti ambapo baraza (madiwani) wanaona ukusanyaji ambapo kwa sasa vinakusanya vijiji ndio njia sahhihi. Kwa hiyo zabuni hipo pending. Sasa inshu ninazotaka ufafanunuzi hapa ni:

1. Je, sheria na kanuni za ununuzi zinaamuaje kuhusu kusitisha zabuni inapotokea mkanganyiko kama huu?
2. Je, wale wazabuni waliokosa vitabu vya zabuni awali haki yao ni hipi? ingawa menejimenti inasema muda wa zabuni ulikishwa pita
3. Je, kuna haja ya kuwajulisha wazabuni kuwa zabuni imezuiwa kwa muda usiojulikana?
4. Je, ni nguvu hipi ya kisheria ambayo baraza linatumia kuingilia mchakato wa zabuni, ingawa labda kulikuwa hakuna uwazi kati yake na menejimenti.
5. Je, iwapo menejimenti na baraza wataamua kuachana na taratibu hizi na kurejea na mfumo wa ukusanyaji uliopo sasa kuna haja ya wazabuni kurejeshewa gharama walizozitumia, pamoja na madhara yake ni yapi iwapo wataamua kushitaki ppra  

Naomba kupatiwa ufafanuzi ili nimshauri Accounting Officer hatua za kuchukua.

raporini

Posts : 1
Join date : 2013-08-14

View user profile

Back to top Go down

Re: Naomba ufafanuzi wa namna ya kusitisha zabuni

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum