Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
December 2018
MonTueWedThuFriSatSun
     12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31      

Calendar Calendar

Statistics
We have 956 registered users
The newest registered user is makoka tailors

Our users have posted a total of 1231 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 3 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 3 Guests

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

SEMINA / WORKOSHOP

Go down

naomba muongozo

Post  Mr.Zubeir H. Zubeir on Thu Aug 15, 2013 6:59 pm

nikiwa kama afisa ugavi na manunuzi katika moja ya taasisi ys serikali ya mapinduzi zanzibar, nakua napata changamoto kali siku hadi siku kwa kule kukosa muongozo wa sheria uliopo kamili kama ule wa Act ya 2004 ya Tanzania bara. kimsingi na kiukweli Act ya tanzania bara ipo sambamba ya inaendana na mazingira ya kufanya kazi za manunuzi ndani na nje ya Tanzania, hali haipo sawa na Act ya Zanzibar ambayo inaonekana kuwapa Fever watendaji wakuu wa taasisi ambao walipaswa kuwa wasimamizi wakuu wa fedha, aidha chombo kilichoundwa kwa ajili ya kuratib na kusimamia harakati za manunuzi na ugavi ndani ya serikali ya zanzibar hakipo active i.e hakuna watendaji walipo compitant kulingana na mahitaji na mazingira ya zanzibar, wapo walio na uhaba wa taaluma ktk fani ya manunuzi, kuna wavivu, wapo wazembe na hata wale waliozoea kufanya kazi kimazoea kama wanakosha vyombo nyumbani kwao. kimsingi na kiutaalamu, idara ya uhakiki mali iliopo ndani ya wizara ya nchi afisi ya raisi fedha uchumi na mipango ya maendeleo ilipaswa kua na sifa, tabia na mwendo kama ule uliopo PPRA wenye uhakika wa kusimamia haki na wajibu wa kila mdau(stakeholder) katika manunuzi.Kiujumla sheria ya zanzibar ni ngumu kuifanyia kazi za manunuzi na hivyo ndo ugomvi wa kila siku kati maafisa wanunuzi na mabosi wao kwa kule ambako maafisa wengi husoma huku dar kutumia Act ya tanzania na kufanya kazi kwa miongozo ya Act ya zanzibar iliosheheni makosa na migogoro ya kimaslahi jambo ambalo huwapa tabu maafisa waliobobea na Act ya tanzania 2004 iliopo sawa kiutendaji. ukiwaelekeza wakubwa wanadai "fanya unaloambiwa kisha utakuja hubiri izo kanuni zako" we kila siku sheria sheria ' kwani umeitunga wewe"? wangapi wanafanya kazi hawafati sheria ndo tuseme hawajui kazi au?

Mr.Zubeir H. Zubeir

Posts : 12
Join date : 2013-07-22
Age : 33
Location : Zanzibar

View user profile http://www.zubeironline.blogspot.com

Back to top Go down

Re: SEMINA / WORKOSHOP

Post  id2013 on Thu Aug 01, 2013 1:39 pm

Mr. Zuberi,
Ulichokisema ni sahihi kabisa kwa platform hii inatakiwa iende mbali zaidi ya hapa kwani inasadia sana katika masuala mazima ya kupsahan habari, kuelimishana. Mimi katika forum hii ninaiona kama mbadala wa semina na workshop ambayo huwa ninaipata nikiwa mezani ofisini au popote ninapokuwa na mtandao kutokana na mada zinazoletwa na kujadiliwa humu.

Binafsi ndio maana nimeomba kwa moderator au wahusika wa kuiangalia forum hii waongeze kipengere hata cha kuweza kuweka kiambatanisho mtu anapokuwa na issue anaweka ili aweze kushare kwenye forum. Mfano ulioutoa kama semina au workshop imetangazwa gazetini basi mtu hata anaweza kuscan kipande cha gazeti ili kuwapasha habari wana forum humu.

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

SEMINA / WORKOSHOP

Post  Mr.Zubeir H. Zubeir on Thu Aug 01, 2013 12:16 pm

Kutokana na umuhimu mkubwa wa kushiriki katika semina mbali mbali zinazoendeshwa na PPRA pamoja na PSPTB ambazo zinalenga kukuza ufanisi na vipaji vya utendaji katika fani hii yenye kuhitaji ujasiri na uchapakazi wa hali ya juu, naomba,napendekeza na pia nashauri kila inapotokezea kufanyika semina hizi alau siku 3 kabla tuwe tunaarifiana hapa au hata kupitia email zetu ili kupata fursa ya kuweza kushiriki katika semina hizi huku tukizingatia kua kama mtaalamu hapati kushiriki katika semina basi utaalamu wake huenda ukapungua nguvu za kiutendaji baada ya mda mdogo.Kiimani ni kua semina zinatupatia nguvu na njia za kuondoa au kupambama na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika shughuli zetu za kila siku katika manunuzi. Nimatumaini yangu kua wenzangu mliopo hapa mtakua mnaleta taarifa za semina kila zinaposikika kwa kuwa wengine inaua sio rahisi kupata taarifa kabla ila tunakuja kuipata taarifa ukipiga simu au kumtembelea mtendaji ofisini kwake unaambiwa yupo semina ya PPRA AU PSPTB siku 3-4

Mr.Zubeir H. Zubeir

Posts : 12
Join date : 2013-07-22
Age : 33
Location : Zanzibar

View user profile http://www.zubeironline.blogspot.com

Back to top Go down

Re: SEMINA / WORKOSHOP

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum