Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
December 2018
MonTueWedThuFriSatSun
     12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31      

Calendar Calendar

Statistics
We have 956 registered users
The newest registered user is makoka tailors

Our users have posted a total of 1231 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 5 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 5 Guests :: 1 Bot

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Go down

Re: KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Post  RSM on Fri Apr 11, 2014 1:44 pm

id2013,

Wakati ulipowasilisha mada hii swali lako kubwa ni kuwa je Katibu ni Mjumbe wa Bodi. Jibu kama ulivyosema ni hapana. Yeye ndiye anayewasilisha mapendekezo kwenye Bodi ya Zabuni kwa hiyo kwa misingi ya utawala bora hawezi kupigia kura mapendekezo yake mwenyewe.

Hata hivyo mimi nataka kuzungumzia suala linguine tofauti. Inaonyesha kuwa Bodi yako inafanya kazi kwa kupiga kura. Mimi inanipa taabu sana nikisikia kuwa mzabuni amepatikana kwa kupigiwa kura. Uchaguzi wa nani ameshinda zabuni sio kura ya maoni ila anachaguliwa kwa vile ametimiza vigezo vyote na yule aliyeachwa ni kuwa hajatimiza vigezo. Itakuwaje baadhi ya wajumbe waone kuwa mzabuni ametimiza vigezo na wengine waone kuwa hajatimiza. Kwangu mimi hiyo ni "red flag" ya rushwa.

Na nini kifanyike kama Katibu ametoa mapendekezo yake ambayo ndiyo anaona yanstahili na wajumbe wametoa uamuzi tofauti? Nadhani katibu hana budi atumie haki yake ya kukubali kutokubaliana kwa mujibu wa kanuni 52 ya Procurement Regulations - GN. No. 446 ya Mwaka 2013.

RSM

Posts : 150
Join date : 2009-08-11

View user profile

Back to top Go down

Re: KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Post  id2013 on Wed Mar 26, 2014 11:49 pm

GWK,
Swali langu kubwa kwako kwanza ni kwamba, kwa maelezo yako na kwa mujibu wa sheria na kanuni yake ya 2013, ''Je neno Mjumbe wewe lina maana gani?, au unalitasfri vipi?,''.

Baada ya kujibu nitarudi ila napenda kusema kwamba Katibu wa Bodi ya Zabuni sio mjumbe wa Bodi ya Zabuni.

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Post  GWK on Tue Mar 25, 2014 8:51 pm

Mimi ni mgeni katika hii forum nimejiunga baada ya kuona mada za kitaaluma zinajadiliwa kwa mapana na zinahusisha wadau wote nchini.

Nikirejea kwa swala la Katibu wa bodi kwamba ni mjumbe wa Bodi au la Jibu ni moja kwamba kwa mujibu wa sheria ya Manunuzi na kanuni zake Katibu wa bodi ni Mjumbe wa bodi. Aidha, Katibu ndiye mtaalam na anatarajiwa kuongoza bodi yake izingatie sheria iliyoiweka Bodi hiyo (Sheria ya Manunuzi). Nasikitika kwamba Katibu wa Bodi anaacha bodi yake ikiuke sheria husika kwa kupiga kura kuteua mzabuni, kubadilisha vigezo ili kupata mzabuni anayetakiwa na bodi ya zabuni n.k

Maoni yangu ni kwamba Katibu simamia sheria inavyotaka baada ya muda mfupi wa kuonyesha msimamo wako watakuelewa na kukuamini (Hakikisha unasimamia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kila siku)

Ni vema wajumbe wa Bodi wakapewa mafunzo ya kuelekezwa utekelezaji wa kazi zao. Bodi nyingine zimeundwa na wajumbe wake hawana mafunzo yoyote na hata hiyo sheria na kanuni hawazisomi. Wanafanya kazi ya umma kwa busara zao tafadhali waandalie mafunzo wanaweza kubadilika.

GWK

Posts : 54
Join date : 2014-03-24
Age : 51
Location : DAR ES SALAAM

View user profile

Back to top Go down

KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Post  id2013 on Tue Jul 30, 2013 4:30 pm

Ndugu wadau,
Naleta mada hii kwa sina uhakika kama ilishazungumziwa siku za huko nyuma na kama ilikwisha tolewa basi mnikumbushe tu nirejee ili mnisadie kile ninachotaka kuandika hapa. Na kama haijawahi kuzungumziwa basi naanza kuuliza yafuatayo;-

Mosi Kwenye muundo wa Bodi ya Zabuni yenye watu wanane ( Cool, Je Katibu ambae ndio mtaalamu wa Manunuzi  ni mjumbe au sio mjumbe?, Je Kama sio mjumbe yeye ana nanafasi gani katika maamuzi ya Bodi ya Zabuni kwenye vikao husika?,

Pili, sambamba na swali la kwanza hapo juu, Je Katibu wa Bodi ya Zabuni mbali na kuwa mtu wa kuchukua muhtsari wa vikao na naweza kusema kazi ya kuchukua muhtsari wa kikao inaweza kufanywa na Sekretariat ya Bodi ya Zabuni ambao ni PMU staff wengine chini ya HPMU, Lakini swali langu linabaki pale pale kwamba kwenye maamuzi ya kikao husika Je Katibu kama Katibu ana muhimu gani achilia mbali kutoa ushauri wa kitaalamu wa nini Bodi ya Zabuni wanatakiwa kuangalia kulingana na sheria ya Manunuzi iliyopo.

Nimeleta mada hii kwa sababu nimekuwa nikikumbana na changamoto za kila wakati Bodi ya Zabuni nilipo kuwa na kawaida ya kusema hasa inapofikia maamuzi wanapiga kura na kusema wewe Katibu huhusiki kusema chochote kwenye kuamua jambo na wao ndio wenye maamuzi hasa wale wajumbe site (6) walio katika jedwali la Pili kipengere cha 2 (b).  Imekuwa kawaida kwangu kila jambo au suala linalojadiliwa kwenye kikao cha Bodi ya Zabuni linaamuliwa kwa kupiga kura na kama ni kura ndio Katibu hahusiki, lakini je kila agenda yafaa kuamuliwa kwa kupigiwa kura katika bodi za manunuzi kwenye vikao vyao?.

Mbali na hilo katika maamuzi hayo wajumbe wamekwenda mbali zaidi kwa kuwa wanakuwa na mamlaka hayo ya kupiga kura na Katibu anaposhauri jambo katika suala hilo wanaloamua kama halielekei kisheria wao hukataa na kusema sisi ndio wenye maamuzi wewe unashauri tu. Sasa katika hili na mimi kama sikubaliani na maamuzi yao ninaweza kuyaingiza kwenye muhtsari kama inavyzunguziwa kwenye jedwali la Pili kifungu cha 3 katika sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 au tena hapo Katibu atakuwa hahusiki kulingana na kifungu hicho?.

Bodi ya Zabuni katika maamuzi yao na kwa kuwa wao ndio wenye maamuzi kwa kutumia kura wamefikia kipindi hata kwenye suala la Mapendekezo ya Kamati ya Uchambuzi kwenye Evaluation Report wanapiga kura kwa maana ya hata kufikia kubadilisha award recommendations kwa kuwa labda mzabuni aliyependekezwa hafahamiki katika soko hata kama kakidhi vigezo vyote. Katibu ukishauri kwamba itakuwa kinyume na utaratibu basi kura hupigwa kwamba hiyo sisi kama Bodi ya Zabuni tumeamua. Na Labda hudiriki hata kurudisha sana Evaluation report PMU lili zirudiwe kwa maana ya kupunguza vigezo (ku-wave) vigezo vingine ili apatikane hasa inapokuwa aliyeachwa ni lowet price ingawa sababu za kumuacaha zipo basi huamuliwa kuandolewa. Hebu hapa tuelimishane vizuri kwa kutumia uzoefu wa vitu kama hivi na si kwa theory tupu. Tulete Case study ili tuzichambue na labda sehemu nyingine zinapotokea hili huwaje? bila ya kuwa na disagrement mpaka kupelekea kuitaarifu mamlaka kwa maamuzi.
Katika suala hili unaweza kujiuliza labda Bodi ya Zabuni haijapata mafunzo hapa mafunzo walishapelekwa na labda waliyapata na kuyaacha kule.

Nawasilisha ili nipate mawazo ya wenzangu wanasemaje na wengine wanisaidie kama lilisha au linawatokea kama hili na kwamba wanafanyaje, hii ni kwa kuborehs tu utendaji wetu wa kila siku.

Nawasilisha.

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

Re: KATIBU WA BODI YA ZABUNI ANA UMUHIMU GANI KATIKA MAAMUZI YA VIKAO VYA BODI YA ZABUNI?

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum