Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 959 registered users
The newest registered user is Mfaume.Bodde

Our users have posted a total of 1232 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 4 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 4 Guests

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

Naomba Ushauri wa maelekezo

Go down

Shukrani kwa majibu

Post  Mr.Zubeir H. Zubeir on Sun Jul 28, 2013 12:22 pm

Napenda kwanza kuwasilisha salamu za shukrani kubwa na za kipekee kwako id2013 kwa kuniweka wazi katika hili lililokua linanitatiza kupia relevant sections from PPA,kiujumla kwanza naomba nikeleze kua mimi nipo ktk taasisi ya jamhuri ya Muungano wa tanzania ambayo ipo zanzibar, wengi wa wazanzibari huku hawaelewi mambo ya sheria katika fani ya manunuzi jambo ambalo wakuu wengi wakizanzibari huzitumia idara za manunuzi kama sehemu za kujinufaisha wao kiuchumi na kimaslahi binafsi,nikiwa kama muajiriwa niloajiriwa kwa fani maalumu ya manunuzi, sijawahi kukubaliana na matakwa ya Accounting officer wangu tangia kuajiriwa katika taasisi hii baada ya kumgundua kua hayupo kutafta Value for Money kupitia taaluma yangu katika taasisi ila yupo kufanya maslahi binafsi ya kiupande wake.Bahati nzuri ameshanigundua kua sipo upande wake kiutendaji jambo ambalo linamfanya kila wakati awe ananiita na kuniuliza "ivi ni kwa nini wewe hutaki kufuata maelekezo ya wakuu wako wa kazi" mimi mda wote nakua namjibu kua siwezi kupinga maelekezo ya mkuu wangu wa kazi nikiamini kua ni moja ya utovu wa maadili ya kazi lakini mkuu wangu unajaribu kuamrisha mambo ambayo yapo nje ya maadili ya kazi na fani yangu sikuelewi unakua na dhamira gani. We ukiwa na maamrisho kama haya nakuomba uwe unaniandikia katika memo ili niweze kutekeleza manake hii ni ofisi ya serikali siku moja nitakuja kufanyiwa Auditing nikiwa na ushahidi wa kimaandishi juu ya maelekeo yako nadhani itaniweka mimi na wewe katika mazingira salama" lengo langu nataka awe anaandika nikaripoti kwa mkuu wa juu yake manake siwez kuripot maneno ya mdomo haipokelewi katika ushahidi baada ya kumjua haelewi analilifanya ila amekata" kuijumla mimi hawezi kuniyumbisha hata kidogo kwa kua ni mtu nilielelewa na kanuni na taratibu pamoja na maadili ya kazi na fani hii takriban miaka 6 sasa,na nipo PPRA siku zote kwa lengo la kubadili na kuchangiana mawazo na wataalamu walipo hapa. How far aje kunibabaisha m2 mwengine kiurahisi?Haiwezekani. NAOMBA ZIKITOKEA SEMINA ZINAZOENDESHWA NA PPRA TUEWE TUNAAMBIANA KWA KUA SOTE NI WADAU WA PPRA TULO NA MALENGO YA KUTAFUTA UFANISI WA KAZI KATIKA TAASISI ZETU

Mr.Zubeir H. Zubeir

Posts : 12
Join date : 2013-07-22
Age : 33
Location : Zanzibar

View user profile http://www.zubeironline.blogspot.com

Back to top Go down

Re: Naomba Ushauri wa maelekezo

Post  id2013 on Tue Jul 23, 2013 3:01 pm

ZUBERI,
Kwanza pole sana yaliyokukuta.
Lakini pia nianze na utangulizi kwamba Accountin Officer wako inaonekana hukumkumbusho kuhudhuria na ama yeye mwenyewe hakuhudhuria ile workshop ya PPRA kwa CEO's wote nchini iliyofanyika Arusha 10-12 July, 2013 iliyokuwa inawapatia mwanga wa utekelezaji wa sheria za manunuzi ya umma katika taasis zao. Na kama alihudhuria basi hicho kitendo cha kufanya evaluation mwenyewe au kubadili evaluation ya kamati amefanya makusudi na naweza kusema kaetnda kosa chini ya kifungu 38 cha sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 kifungu hiki kikisomwa sambamba na kile cha kanuni ya 8 ya mwaka 2005 kinachozungumzia maadili ya Afisa wa umma wanaposhuhgulikia masuala yote ya manunuzi na uuzaji wq vifaa chakavu kwa njia ya zabuni. Accounting Officer wako kama yeye Afisa wa Umma alitenda kosa katika kifungu hiki kwa kutokuwa mwaminifu katika kushughulikia manunuzi ya taasisi yake. Pia kifungu cha 28 (5) cha sheria ya manunuzi 2004 kinakataza mtu kama accounting officer kuwa na kampuni yake kushiriki zabuni hapo kwake vinginevyo ange-declare interest kwanza wakati wa mchakato .

Pili, ZUBERI NAOMBA sasa nianze na yafuatayo;-
Mosi, Je wewe ulikuwa mmojawapo wa wanakamati ya evaluation?, Kama ulikuwemo basi ulitenda kosa chini ya Section 38 ya PPA 2004,

Tatu, je composition yako ya evaluation commitee ilizingatia Section 37 (4) na 37 (6)?

Nne, Je Evaluation Report unayoizungumzia iliidhinishwa na Bodi ya zabuni kwa mazingira yeyote yale?, hapoa nimeona unazungumzia Accounting Officer kupelekewa ripoti hiyo na sio Tender Board, Je aliibadili baada ya Bodi ya zabuni kuidhinisha au kabla?, kwa mazingira yeyote yale Accounting Officer anabanwa na kifungu cha 31 (1) cha PPA 2004 na kwa hiyo Tender Board wanahaki ya kuitaarifu PPRA kuhusu suala hilo chini ya Section 30 (4) ya PPA 2004.

Tano, Je ZUBERI wewe ndio unakagua vifaa vyote unavyovinunua?, kama unafanya hivyo mnakiuka kanuni ya 127 ya mwaka 2005 toleo la Serikali namba 97 inayozungumzia kuundwa kwa kamati ya kukagua na kupokea vifaa vinavyonunuliwa. Lakini pia Public Finance Regulations, 2001, Revised 2004 under Regulation 191 (2) states that '' The task of receiving and checking stores shall be carried out by an officer other than the one who placed the orders and authorised payment for the supplies.''

Kwa manzgira haya ninavyofikiri mimi ndio kilipelekea kifungu 127 kuwekwa, kwa hiyo bado mna makosa katika taratibu za kupokea vifaa vyenu.

ZUBERI nini kifanyike?

Nakushauri katika suala zima la huo mchakato wako na evaluation report hii, nakuomba ufanye yafuatayo
(i) Kama nilivyoeleza juu hapo katika kipengere cha nne (kama bodi ya zabuni lilipitia na kuidhinisha mapendekezo ya evaluation commitee) na Accounting Officer akabadilisha bila taarifa ya Bodi ya zabuni na kwa manufaa yake, BASI BODI YA ZABUNI ITUMIE KIFUNGU 30 (4) CHA PPA 2004 kuiarifu Mamlaka (PPA) kuhusu uvunjivu wa sheria hii
(ii) Kama wewe ni katibu wa bodi ya zabuni na kwamba ndio HPMU unaweza kuiarifu Mamlaka (PPRA) moja kwa moja kwa kutumia Kifungu 35 (d) kuhusu suala hilo na kwa kuwa tayari umesema hutasaini ripoti hiyo na kwa kweli ndipo niliposhangaa kwa nini usaini evaluation report ya kamati nyingine?..

Napenda kuwasilisha kwa hayo kwanza.

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

Naomba Ushauri wa maelekezo

Post  Mr.Zubeir H. Zubeir on Mon Jul 22, 2013 11:09 am

Mkuu wangu wa taasisi anamiliki kampuni ya usambazaji wa vifaa vya ofisini(Stationery) ,Nimeitisha zabuni na moja ya sapplier walokuja kuchukua tenda ni kampuni yake, wakati nafanya Evaluation nikiwa kama Katibu anakuja na kauli  ya " Unajua Mr.Zubeir hapa ni mjini na waswahili siku zote huwa wanasemaga kua mji una masharti yake si ndio! nikaitikia "ndio mkuu wangu ila naona bado sijapata mantiki ya msemo huu kwa mujibu wa mazingira ya hapa nilipo! alianza kujichekesha na mwaisho ilibidi aniambie kuna kampuni inaitwa------------(siwezi kuiweka hapa) iyo ndo kampuni tunayoitumia hapa mda mrefu kabla kuja wewe kwa masuala ya kuleta stationery, kwaiyo evaluation yako ujue unafanyaje" bahati nzuri hata mzunguko wa pili katika mizunguko ya evaluation haikufika na mimi nikasemahapa kama wameniajiri kama mtaalamu wa hii fani, siwezi kuweka dosari katika fani yangu hasa nikikumbuka maadili "Ethical conducts in Procurement" timu ya evaluation ikaandika ripoti pamoja na recomendation juu ya mzabuni alostahili kupewa zabuni akapelekewa yeye akiwa kama Accounting Offser,alichokifanya ni kumtumilia mmoja ya wajumbe wenyeji(waliokua hawana sifa na vigezo vya kitaalamu vya kushiriki katika tathmini hile) wa taasisi walokuemo katika evaluation commetee na kumuambia ampatie soft copy ya Evaluation yetu na wakampatia, bosi akafanya anavyotaka yeye na mzabuni alomtaka yeye ambae ni kampuni yake ndo aloirecomend kua ipewe tenda,List ya kuwataka wajumbe waweke tena signature upya kwa mujibu wa evaluation ripot mya ikafika kwangu ikiwa watu wote wameshaweka signature ispokua mimi tu katibu wa tender bord na mjumbe wa kamati ya tathmini, mimi nimekataaa kueka signature kwa kutoa sababu kwa mujibu wa taaluma yangu inavyonielekeza na matokeo yake nimepewa barua ya kuonywa kua napinga maelekezo ya wakuu wangu, siku ya pili stationery zimeletwa nikatakiwa niende kufanya Inspection nimekataa kwa kutoa ufafanuzi wa taluma yangu, zimewekwa stoo na zimeshaanza kutumika. Je nifanyeje Procurement Officer?

Mr.Zubeir H. Zubeir

Posts : 12
Join date : 2013-07-22
Age : 33
Location : Zanzibar

View user profile http://www.zubeironline.blogspot.com

Back to top Go down

Re: Naomba Ushauri wa maelekezo

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum