Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 959 registered users
The newest registered user is Mfaume.Bodde

Our users have posted a total of 1232 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 4 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 4 Guests

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Go down

Re: KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Post  RSM on Wed Jul 17, 2013 3:52 pm

id2013

Nimefurahishwa sana na mchango wako ambao umejaribu kulichambua kwa kina tatizo la bei na nini kifanyike. Ila ndugu yangu hujaongelea jambo lingine ambalo ni muhimu, hata hao wanaonunua kwa cash na kwa bei ndogo kuna wakati bidhaa wanazonunua ni feki na hazina garantii tofauti na ambavyo Taasisi za Umma zinaponunua zinavyosisitiza hilo liwepo kwa kuomba Manufacturer's Authorization kudhibitisha kuwa bidhaa sio feki na kupewa guarantee. Yote hayo vile vile yanachangia wakati mwingine kwa bei za Taasisi za Umma kuwa juu pamoja na zile nilizozitaja awali.

Ni kweli tunahitaji maboresho makubwa kwenye mfumo wa ununuzi wa bidhaa mtambuka ambao wenzetu wa GPSA wanauendesha, na ni kweli ukifikia kiwango cha ufanisi kinachotakiwa utazisaidia Taasisi nyingi za Umma kupunguza gharama za ununuzi. Ila mimi naona chini chini kuna watu wanaupiga vitu utaratibu huu kwani labda utawapunguzia ulaji.

Hivyo maboresho tunayoyataka mimi naona ni "Technical Solution" kwa tatizo ambao linahitaji watu kubadili tabia. Maboresho yote ya mfumo hayatakuwa na tija kama watu hawatabadili tabia za (1) kuanzisha kampuni feki kwa lengo la kuuibia serikali kupitia zabuni, (2) kuuuza bidhaa feki, za ujazo mdogo na ubora mdogo (3) kuomba hongo kutoka kwa wafanyabiashara na (4) kuchelewesha malipo ya wazabuni hata pale pesa zinapokuwepo.

PROFESSIONALS TUBADILI TABIA NA TUONYESHE NJIA. Tunayo dhamana kubwa sana kwa wananchi wa Taifa hili. Tusije tukastukia siku moja wananchi wakituchapa viboko hata kwenye makaburi yetu.

RSM

Posts : 150
Join date : 2009-08-11

View user profile

Back to top Go down

Re: KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Post  id2013 on Wed Jul 17, 2013 3:00 pm

RSM/SELEMAN
RSM kama alikuwa na jibu kama nililokuwa nalo mimi. nimependa sana majibu yote 3 aliyotoa RSM lakini pia nitafurahi sana kama majibu haya au hoja hii itakuwa imepata ufafanuzi na kujadiliwa kwenye semina zile zilizofanyika Arusha kwa wakuu wetu wa kazi (Board of Directors na CEO's  wa PE's) hivi karibuni. Hii kwa sababu kila lawama zimekuwa zikipelekwa kwetu Professional kana kwamba kweli vitu hivi tunavisababisha sisi.

Kuhusu suala la bei kutofautiana mimi cha kuongeza ni kwamba ni sawa GPSA wanafanya kazi kubwa na nzuri ila wanatakiwa sasa wawe na utafiti endelevu kuhusu bei za bidhaa kwenye soko la ndani hata na lile la ndani ili kuwa na ufahamu hata kama wanafanya wastani wa bei za bidhaa kutoka kwa wazabuni wa ndani watakuwa wanelewa hizo bei ni realistic au hapana kutokna ana wao pia wamefanya hizo gharama za kuagiza mpaka kufikisha mzigo nchini na kwa maana zile grey market prices kuzipunguza.Hii itasaidia hata serikali kufahamau na kufanya maamzui mengine kwa kuwa GPSA wanajua gharama halisi za kuagiza Kumputa kutoka nje au kwa international delears au manufacturer mpaka inafika na nchini ukijumulisha kodi zote, sasa suala linabaki margin ya profit inayowekwa  na wafanyabiashara haiwi ile ya superprofit ambayo ndio inayopelekea kulalamikiwa na umma kwamba bei za zabuni a ghali kuliko ile ya direct purhase by Cash.

GPSA pia wapanue wigo wa Sampling ya kuchukua bei kwa sababu haieleweki ni kwa kiasi gani na kwa umbali gani hizo bei wanazipata kutoka sokoni. Ni lazima kuwa na benchmark kwamba kati ya wafanyabiashara wa komputa labda 1000 waliopo Tanzania kujumulisha na wale Dealers, GPSA wametumia sample size ya kampuni labda 200 au 500 au 700 kutafuta wastani wa bei hizo ili kuondoa mwanya mkubwa wa tofauti hizo za bei. Kwani sample size kubwa katika hesabu za takwimu ndio inaklupataia majibu sahihi kwa maana kama umechukua idadi kubwa ya kuchukua bei kwa wafanyabiashara hao basi bei zake zinakuwa almost sawa regardless source of supply huyu mfanyabiashara wa nchini katoa wapi bidhaa hiyo. Hiyo inatosha kumpa jibu GPSA na mimi kwa hilo sina uhakika kama linafanyika hivyo na kama linafanyika hivyo kwa maana ya kuchukua wigo mkubwa wa sample size basi litasaidia kabisa kupunguza huo utofauti kwani bei za GPSA zitakuwa ''almost equivalent to the market price''.

Mimi binafsi mfumo wa GPSA naukubali sn na nimeupenda mno ingawa unahitaji kuboreshwa kila wakati. Kwanza mfumo huu umeturahisishia sana sisi watendaji katika vitengo vya PMU na ofisi nzima kwa maana ya kuwa Efficient kwa kupata vifaa kwa haraka bila kupitia mchakato wa muda mrefu wa kununua vitu ambavyo ni repititive, routine and with small value, umepunguza pia internal tendering cost, hasa kuwa na vikao vya Bodi ya zabuni kila wakati kuidhinisha ununuzi wa vifaa vya CUIS labda pale unapotumia Mini Competition ingawa si lazima kuitisha kikao cha kukaa Tender Board kwani Circular Resolutions ipo. Kwa ujumla inahitajika elimu kubwa kwa watendaji wa vitengo vya PMU, PE's, Umma kwa maana pia ya wafanyabiashara kuhusu kasoro ndogondogo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mfumo wa GPSA lakini kwa ujumla mimi nasema ni mzuri.

id2013

Posts : 50
Join date : 2013-07-17

View user profile

Back to top Go down

Re: KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Post  RSM on Thu Jun 20, 2013 7:24 pm

Seleman,

Sijakuelewa, una maana tuanzishe Wakala mpya wa Manunuzi Tanzania? Au una maana Je kuna haja ya kuendelea kuwa  na Wakala wa Manunuzi Tanzani tuliyenaye sasa ambaye ni GPSA?

Kuhusu suala la bei ya viti dukani kuwa shs 20,000 wakati bei ya GPSA ni shs 50,000 nadhani hilo ni suala lenye mjadala mrefu. Nitatoa hoja zangu kama ifuatavyo ili kuibua mjadala kuhusu tofauti ya bei ya dukani na bei zinazopatikana kutoka kwa suppliers walio na mikataba na GPSA


  1. Kuhusu kiti, viko vya ubora tofauti, je bei unayoitaja inazungumzia kiti chenye ubora ule ule? Si tunajua kuna viti vya plastic ambavyo inabidi uweke viwili viwili ndio uweze kukaa kama hutaki kuvunja mgongo?
  2. Unapokwenda kununua vitu dukani unalipa in cash. Ukinununua kama Taasisi za Umma unataka uletewe hadi ofisini na kisha ulipe sio kipindi kisichopungua mwezi mmoja. Kuna wakati Taasisi zinachelewesha kulipa hata zaidi ya mwaka mmoja. 
  3. Kwenye Taasisi za umma baadhi ya watu wanataka walipwe 10% ili waagize vifaa au huduma kutoka kwa supplier mwenye mkataba na GPSA. Zipo Taasisi zingine cheque ya malipo haitoki mpaka watu wa uhasibu wakatiwe kitu kidogo n.k. Yote hayo yanapelekea wazabuni kujihami kwa kuweka bei za juu kwenye zabuni za Taasisi za Umma ukilinganisha na pale unapokwenda kama mtu binafsi kununua kwa cash.


Tufanye nini. SULUHISHO LA TATIZO HILI NI KWA WATENDAJI KUWA WAADILIFU NA KUTOOOMBA 10% na vile vile TAASISI KUHAKIKISHA KUWA ZINALIPA WAZABUNI KATIKA MUDA MFUPI IWEZEKANAVYO.

RSM

Posts : 150
Join date : 2009-08-11

View user profile

Back to top Go down

KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Post  IS-HAQ SELEMAN on Tue Jun 18, 2013 6:24 pm

WAZALENDO KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA ,IKIWA BIDHAA ZINAZOODHORESHWA BEI YAKE NI KUBWA UKILINGANISHA NA BEI HALISI YA SOKONI .NINI MANTIKI YA WAKALA KWA MFANO KITI CHA KAWAIDA CHA PLASTIC BEI GPSA NI WASTANI WA TSHS.50,000/= WAKATI SOKONI NI WASTANI WA TSHS. 20,000/= VALUE FOR MONEY IPO WAPI HAPO .

IS-HAQ SELEMAN

Posts : 1
Join date : 2013-06-18

View user profile

Back to top Go down

Re: KUNA HAJA YA KUWA NA WAKALA WA MANUNUZI TANZANIA

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top

- Similar topics

 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum