Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
December 2018
MonTueWedThuFriSatSun
     12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31      

Calendar Calendar

Statistics
We have 956 registered users
The newest registered user is makoka tailors

Our users have posted a total of 1231 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 6 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 6 Guests :: 1 Bot

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

NI NANI ALIKUFUNDISHA

Go down

Re: NI NANI ALIKUFUNDISHA

Post  GWK on Thu May 08, 2014 7:06 pm

Kaka,
Swali hili ni la siku nyingi na uchangiaji wake ni mgumu. Hata hivyo najaribu.
Wakati naanza kazi ya kuajiriwa (Nikiwa na Diploma) nilikuwa napata mshahara mdogo sana (Tshs 6,180/=) ambao haukuweza kunifikisha mwisho wa mwezi kwa namna yoyote kwani kwa mfano Godoro (3.5'x6'x6" lilikuwa linauzwa sh 18,000/= sawa na mshahara wa miezi mitatu. Redio kaseti panasonic ilikuwa sh. 34,500/= (Mshahara wa miezi mitano), Baiskeli 52,000/= (mshahara wa miezi 9). Kwa maana hiyo pamoja na kuwa nilisoma hadi kidato cha nne na kusomea kazi chuoni kwa miaka mitatu pamoja na kupata mafunzo ya jeshi kwa mwaka mzima sikuweza kununua mahitaji ya lazima na ya msingi kwa kutumia mshahara niliokuwa nalipwa. Namshukuru mkuu wa kazi aliyeliona hilo na kuwa anatupa allowance ya shs 9,000/= kwa mwezi ambayo ilisaidia kwa chakula.

Kwa upande mwingine wenzangu niliomaliza nao shule ya msingi na wakawa kwenye biashara walikuwa na maisha mazuri na hawakuwa na taabu ya mahitaji ya muhimu na kimsingi walikuwa wanasaidia wazazi wao vizuri (mimi sikuwa na uwezo huo). Maneno kijijini kulinganisha vijana waliosoma na ambao waliishia darasa la saba yakawa makubwa na msemo wa kushindwa masomo sio kushindwa maisha ukawa na maana kubwa na huenda kukatisha baadhi ya vijana morali wa kusoma kwa bidii.

Kwa kuwa sikuwa sehemu inayonikutanisha na wateja sikuwa na namna yoyote ya kupata kitu cha ziada toka kwao. Nilijitahidi sana kufuata maelekezo ya Dini na kwa kweli ilisaidia kunituliza kisaikolojia na nikaendelea na kibarua hadi leo ambapo kwa kweli hali ni nzuri sana ukilinganisha na miaka hiyo niliyoanzia kazi.

Maoni kwa waajiri/waajiriwa:
1. Mlipe mfanyakazi wako ujira unaotosha mahitaji ya lazima ya kila siku. La sivyo ataingia njaa itamfanya aangalie sehemu anayoweza kupata kipato cha kuziba (bridging the salary gape)
2. Waajiriwa tuwe wakweli kwa waajiri wetu ili kwa pamoja tujenge uchumi wetu, Taasisi na Nchi kwa ujumla

Asanteni

GWK

Posts : 54
Join date : 2014-03-24
Age : 51
Location : DAR ES SALAAM

View user profile

Back to top Go down

NI NANI ALIKUFUNDISHA

Post  freddy.mbeyella on Tue Nov 13, 2012 10:41 pm

Jamani hakuna mchango wowote kwenye hili! Au sijaeleweka? Napenda kueleza kwamba hakuna jibu sahihi, kuna wewe unasemaje kwenye hili! Mnajua ndugu zangu sote ni wahanga wa waliotutangulia! Yaani karibu kila jambo tumejifunza mahali fulani. Suluhu kwenye maswala ya tabia ni kufahamu wapi umetoa au umepata!Kwa kufahamu ulikopata unaweza kupata suluhu siyo kwenye hili tu bali kwenye mambo mengine pia. Hata hivyo silazimishi jibu. Swali/ fumbo linaweza kudumu bila jibu mradi ujumbe unafika!

freddy.mbeyella

Posts : 74
Join date : 2009-08-25

View user profile

Back to top Go down

NI NANI ALIKUFUNDISHA

Post  freddy.mbeyella on Wed Jun 06, 2012 2:48 pm

Swala la ukosefu wa uadilfu limekuwa likijadiliwa kwa mapana na marefu katika nyanja mbalimbali kuanzia katika familia, dini, vyombo mbali mbali n.k. Uharifu kwa ujumla wake umeundiwa taasisi mbali mbali kukabiliana nalo mfano, polisi, mahakama, magereza, PCCB, Tume ya Maadili n.k. Lakini hali inaelekea hali kutobadilika. Nimekuwa nikiuliza maswali mengi kuhusu hili jambo lakini sipati jibu. Hususani nini chimbuko lake na nini kifanyike. Natambua utafiti mwingi umefanyika na unaendelea kufanyika kutafuta ufumbuzi wa swala hili na kunabadhi ya nchi zimefanikiwa kwa kiasi fulani kulitokomeza. Ukweli unabakia pale pale kuwa ni changamoto kwasababu lipo katika maisha yetu ya kila siku. Jambo hili limetoka mbali kizazi kimoja hadi kingine na linamhusu kila mtu kwa namna moja au nyingine. Naamini kila mtu kwa kujua au kutojua amewahi kufanya tukio la kukosa uadilifu. Mfano tukiwa wadogo wengi tuliramba sukari kwa wizi! Huu ni mfano mdogo. Hivi ni unadhani ni nani alikufundisha kudokoa? Hali hiyo hiyo imeendelea hadi ukubwani. Jee ulipoajiliwa ulifundishwa kila kitu kuhusu kazi yako yaani pande zote? Nani alikufundisha mbinu za kupata bila halali? Jee ulijisikiaje kwa mara ya kwanza kupata bila halali ?Pengine sasa umefanikiwa kuacha jee umefanyaje? Jee baada ya kuacha unajisikiaje na kwanini?

Ndugu wachangiaji mada hii naiwalisha kwa nia ya kujadili na kuchangia mawazo yanatokana na uzoefu wa maisha. Natambua ni vigumu kusema moja kwa moja kwani jambo lenyewe halipendezi! Lakini naamini katika kubalidiishana mawazo tunaweza kupeana moyo na mbinu ya kuachana na mbinu chafu bila kutishwa na sheria. Unaweza kuchangia kwa kutoa mfano usio halisi. Unaweza pia kujadili moyoni na kuona ukweli mkubwa zaidi.

freddy.mbeyella

Posts : 74
Join date : 2009-08-25

View user profile

Back to top Go down

Re: NI NANI ALIKUFUNDISHA

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum