Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 959 registered users
The newest registered user is Mfaume.Bodde

Our users have posted a total of 1232 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 3 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 3 Guests :: 1 Bot

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Go down

Re: kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  GWK on Thu May 29, 2014 5:33 pm

Wadau wote mliochangia mada hii, nawashukuru kwa mchango wenu unaoonyesha ni kwa nini matengenezo ya magari ya Serikali ni ghali kuliko watu binafsi. Ni kweli Serikali inatengenezea magari yake kwenye gereji zilizosajiliwa na sio chini ya mwembe, malipo yanaweza kuchukua muda mrefu (time value of money), nk.

Pamoja na hayo, tusikatae ukweli kwamba gharama za utengenezaji wa magari ni kubwa kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu, matengenezo na ukaguzi kufanywa na idara moja ambayo huwa inacharge ada yake kulinagana na gharama za vifaa. Nimeona wakiwa wameandika kwenye profoma invoice; N 70 dry battery Shilingi 390,000/= wakati dukani ni shilingi 250,000/=. Ili kupunguza gharama hizi, ningependekeza kwa wadau wanaoandaa sheria, kanuni, miongozo yafuatayo;

1. TEMESA isifanye kazi ya matengenezo. Kazi yake iwe kukagua kabla gari halijatengenezwa na baada ya matengenezo hii itasaidia sana kuhakikisha gari limetengenezwa kikamilifu na hakuna udanganyifu (Haiwezekani kukagua, kutengeneza na kuweka gharama stahili bila kuwa na upande mwingine unaokagua)
2. Charge ya TEMESA iwe lumsum, isiwe inakokotolewa kwa asilimia ya gharama za vifaa. Hii itaondoa kishawishi cha kuongeza gharama na idadi ya vifaa kwa lengo la kufanya charge yao kuwa kubwa.
3. Ofisi za TEMESA zijengewe uwezo. wafanyakazi hawajapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kulinagana na technologia iliyopo, vifaa vyao ni duni, ofisi zimechakaa na kwa ujumla wafanyakazi wamekata tamaa. KATIKA HALI HII NATEGEMEA HUDUMA DUNI NDIO ITAKAYOTOLEWA
4. Wafanyakazi wapatiwe mshahara wa kutosha kujikimu. itasaidia kupunguza matumizi hewa. (Fanya utafiti kwenye vituo vya mafuta uone namna wanavyobadilisha mafuta na fedha kwa ajili ya kujikimu) watashindwa vipi kuongeza bei ya matengenezo ili wapate ziada kwa ajili kujikimu?

Tukubali kwamba matengenezo na hata uendeshaji wa magari ya Serikali ni ghali kwa namna yoyote ukilinganisha na gari binafsi katika hali zote sawa na ya Serikali. Tukikubali tunaweza kuithibiti na hivyo kupunguza mzigo kwa Serikali yetu. Tukikataa tutakuwa tumekataa ukweli

GWK

Posts : 54
Join date : 2014-03-24
Age : 51
Location : DAR ES SALAAM

View user profile

Back to top Go down

Re: kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  allen mmbaga on Wed Mar 05, 2014 1:27 pm

kikubwa nikwasababu yanatakiwa yafanyiwe matengenezo ya uhakika kama ni kifaa chakubadilisha kinatakiwa kiwe kipya sio used.zaidi ya hapo kingine kinachosababisha gharama ni negotiation .ninaamini kama procedures za kufanya negotiation zikifatwa kama inavyotakiwa matengenezo hayo hayataonekana kama ni yagharama kubwa kwa sababu value of money itakuwa ime take place .

allen mmbaga

Posts : 1
Join date : 2014-03-04

View user profile

Back to top Go down

kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  Maduhu on Tue Feb 04, 2014 8:12 pm

Rahisi sana kwa Mtizamo wa kawaida, Serikali haibabaishi kwenye Suala la utengenezaji, inatumia Garage zinazolipa Kodi zenye wataalam wanaolipwa vizuri na wanaelewa nini wanafanya, Vipuri hubadirishwa Vipya badala ya 'used' isiyojulikana 'expire date' yake itakuwa lini; na zaidi ya hapo mkataba wa matengenezo hufanyika mwanzo wa mwaka ukiweka mabadiliko yoote yanayoweza kutokea ndani ya mwaka husika, malipo pia wakati mwingine hayafanyiki kwa wakati. Kumbuka hii ni biashara.

Ukitaka kujua tofauti ya bei kwa garage za kawaida na zile nilizozitaja juu nenda sehemu kama Toyota Tanzania, CFAO Motors, Nduvin nk. (just to mention).

Nakubaliana pia na hoja za nini hasa kinachotumika kulinganisha sehemu hizi mbili kwa kuzingatia aina ya uharibifu na mahala hizi gari zinapofanyiwa matengenezo.

Maduhu

Posts : 21
Join date : 2010-08-02

View user profile

Back to top Go down

Re: kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  Deogras Karol. on Tue Jan 21, 2014 2:46 pm

fungogood wrote:Safari za viongozi wa serikali zinatakiwa kuwa za uhakika na salama hivyo ni vizuri kugharamia sana kuondoa sintofahamu nyingi zinaweza kutokea barabarani kutokana na kufeli kwa vyombo vya usafiri, hivyo lazima kiasi kikubwa cha pesa kitumike...
Nafikiri ambacho anauliza hapa ni kuwa, ukijaribu ku compare bei ya matengenezo ya gari za serikali na gari binafsi, gari za serikali gharama yake ipo juu sana, this is like nguo unayonunua Kariakoo gharama yake ni tofauti na utakayonunulia Posta, japo nguo ni hiyo hiyo!
kuna nini hapa??

Deogras Karol.

Posts : 5
Join date : 2014-01-15
Location : Dar es Salaam

View user profile

Back to top Go down

Kutumika kwa fedha nyingi kwenye matengenezo ya magari ya Serikali-sababu

Post  fungogood on Fri Dec 06, 2013 9:46 pm

Safari za viongozi wa serikali zinatakiwa kuwa za uhakika na salama hivyo ni vizuri kugharamia sana kuondoa sintofahamu nyingi zinaweza kutokea barabarani kutokana na kufeli kwa vyombo vya usafiri, hivyo lazima kiasi kikubwa cha pesa kitumike...

fungogood

Posts : 3
Join date : 2013-07-24
Age : 32
Location : DAR ES SALAAM

View user profile

Back to top Go down

Re: kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  CGM-''Ng'wigi'' on Mon Jun 11, 2012 10:49 pm

Nicholaus,
Suala la gharama kubwa katika utengenezaji wa magari ya serikali linategemea sana kama walivyotangulia wenzagu kusema unaupima katika kigezo kipi.
Mfano, Gharama ya kutengeneza gari sehemu iliyobonyea au kugongwa (Body Work) ni lazima iwe tofauti na gharama yeyote ile na ile ya maintennace tu ya kawaida ya kurudishia vifaa vilivyokufa kwenye gari. Hata hivyo Body work nayo pia itatofautiana kulingana na ukubwa wa tatizo kwenye gari hiyo.

Cha msingi tunapozungumzia gharama ya matengenezo ni lazima tuimarishe hadidu za rejea (TOR/STATEMENT OF REQUIREMENTS) katika matengenezo tunayozungumzia ili tuwe na uwiano na kitu cha kulinganisha, na ndio tufikie kusema kwamba katika utengenezaji wa magari ya serikali labda katika Body Work/ au maintenance/repair za aina fulani ni a ghali sana. Hapo tutaweza kutoa mchango mzuri na uzoefu katika suala hili.
Tafadhali nabaki.

CGM-''Ng'wigi''

Posts : 16
Join date : 2011-10-02

View user profile

Back to top Go down

kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  freddy.mbeyella on Wed May 30, 2012 12:46 pm

Swali lako ni la msingi ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi ili liweze kujibiwa/kujadiliwa kwa ufasaha. Swala la bei kubwa/ gharama kubwa linategemea unalinganisha na nini? Matengenezo yanafanyika wapi? Umri wa gari n.k

freddy.mbeyella

Posts : 74
Join date : 2009-08-25

View user profile

Back to top Go down

kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  Nicholaus on Fri May 04, 2012 3:25 pm

Naombeni mawazo wadau kwanini magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei gali sana

Nicholaus

Posts : 1
Join date : 2012-05-04

View user profile

Back to top Go down

Re: kwanini matengenezo ya magari ya serikali yanatengenezwa kwa bei za juu kuliko ya binafsi

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum