Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 959 registered users
The newest registered user is Mfaume.Bodde

Our users have posted a total of 1232 messages in 347 subjects
Who is online?
In total there are 4 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 4 Guests :: 1 Bot

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 49 on Fri Jul 06, 2018 7:06 am

MATENGENEZO YA MAGARI

Go down

Re: MATENGENEZO YA MAGARI

Post  Rutaihwa on Thu Mar 15, 2012 5:20 pm

Mbafu,
Hii Changamoto ilinikumba lakini mie niko makao Makuu ya mkoa ndio maana nikaanzisha mjadala huu lakini kupitia vikao vya Bodi ya Zabuni,Kamati ya Ushauri ya Mkoa/Wilaya,Menejimenti unaweza ukapata ufumbuzi.


Ni kweli kabisa suala la Magari kutengenezewa TEMESA liko katika Kanuni za Ununuzi
1.Magari yaliyopo Mkoani lazima yapate kibali chaTEMESA kutengenezewa Karakana Binafsi
2. Si Busara Kutoka Wilaya ambayo hipo Km nyingi kama 500 kufuata huduma ya TEMESA kwa ajili ya service ya Kawaida ambayo ingegharimu takribani Tshs 300,000/= kama ingefanyikia Wilayani. Kwa kupeleka gari hili TEMESA utatumia lita 167 sawa na shs 2300 x 167 = Shs 384,000.00 ongeza gharama ya TEMESA ambayo inaweza kuwa Tsh 280,000.00 Hivyo basi gharama za matengenezo itakuwa ni TSH 664,100.00 kwa TEMESA. Hapa hakuna thamani ya fedha. Kitu cha msingi TEMESA au Wizara ya Ujenzi Itimize Matakwa ya Sheria Na Kanuni za ununuzi za kuwa na karakana Teule kwa Kila Wilaya. Aidha, kwa kuwa Bodi za Zabuni za kila PE zipo kinachotakiwa kwa maoni yangu inapotokea kutengeneza magari Wilayani zihusishwe Katika kutoa uamuzi na kueleza Sababu za Kuridhisha. mfano Umbali, gharama, UJENZI/TEMESA kushindwa kutekeleza Sheria ya kuwa na Karakana Teule .NK.
3. Kwa suala la Magari ambayo bado yapo chini ya mkataba na Muuzaji, Nashauri mkataba wa kisheria mliokubaliana Uzingatiwe.Ili Serikali/wewe isije ikapata Hasara endapo kifaa Muhimu na cha gharama kubwa kama Injini, block Nk kitaaribika kabla ya muda wa mkataba kuisha ambacho ingebidi kinunuliwe na Muuzaji kama ungefuata masharti ya muuzaji.

Mathias Mbafu wrote:RSM Ni kweli kabisa,

Tatizo kubwa la sisi watanzania ni kuchanganya siasa na taaluma nadhani imefika wakati tunapaswa kutenganisha siasa na mambo yanayohitaji taaluma. Mbaya zaidi ni pale ambapo mtu anashindwa kutenganisha Chepe (Spade) na kijiko, hadi inapelekea kuiita chepe ni kijiko kikubwa (Let us call a spade a spade and not a big spoon).

Kwa hiyo The truth shall always prevail.
[list=1][*]


Last edited by Rutaihwa on Thu Mar 15, 2012 5:42 pm; edited 1 time in total (Reason for editing : MAREKEBISHO)

Rutaihwa

Posts : 58
Join date : 2011-09-29
Age : 51

View user profile

Back to top Go down

MATENGENEZO YA MAGARI

Post  Mathias Mbafu on Wed Mar 14, 2012 8:17 pm

RSM Ni kweli kabisa,

Tatizo kubwa la sisi watanzania ni kuchanganya siasa na taaluma nadhani imefika wakati tunapaswa kutenganisha siasa na mambo yanayohitaji taaluma. Mbaya zaidi ni pale ambapo mtu anashindwa kutenganisha Chepe (Spade) na kijiko, hadi inapelekea kuiita chepe ni kijiko kikubwa (Let us call a spade a spade and not a big spoon).

Kwa hiyo The truth shall always prevail.

Mathias Mbafu

Posts : 6
Join date : 2012-03-09

View user profile

Back to top Go down

Re: MATENGENEZO YA MAGARI

Post  RSM on Wed Mar 14, 2012 6:31 pm

Mbafu,

Nadhani huu ni ukiritimba tu wanaouleta TAMESA. Nadhani ni wakati muafaka wao kukubali kuwa ofisi zao za mikoani haziwezi kufanya matengenezo ya magari kutoka wilayani na badala yake waidhinishe magereji kwenye ngazi ya Wilaya ili matengenezo yafanyike huko. Na hilo liko ndani ya Sheria na Kanuni.

RSM

Posts : 150
Join date : 2009-08-11

View user profile

Back to top Go down

MATENGENEZO YA MAGARI

Post  Mathias Mbafu on Wed Mar 14, 2012 6:09 pm

Ni ukweli usiopingika kuwa sheria na kanuni za manunuzi haziendani kabisa na uhalisia wa mazingira tuliyonayo, kwa mfano umbali wa kutoka wilaya ya Njombe hadi Makao makuu ya Mkoa wa Iringa ambako TAMESA Mkoa wa Iringa ndiko waliko unaleta gharama zisizo za msingi kama PEs zilizopo Njombe, Makete na Ludewa zitakwenda kufanya Matengenezo ya Magari TAMESA .
Jambo la Pili ni ukweli usiopingika Kuwa Manufacturer/Dealer wa Kampuni husika iliyosupply gari hutoa warrant period ya kuhakikisha kila kilometa zinapofika za kufanya matengenezo ya magari basi PE atapaswa kupeleka gari hilo kwa Dealer ili aweze kufanya matengenezo hadi muda/kilometer ambazo zilikuwa zimewekwa zikiisha ndipo PE ataendelea na utaratibu wa kawaida wa kufanya matengenezo ya magari.
Hivyo nashauri TAMESA wajaribu kupita mawilayani ili kuweza kuwakagua wenye magereji binafsi na Dealers ambao watafuzu kuwa na vigezo vinavyostahili wapewe vibali ili waweze kuendelea kutoa huduma ya matengenezo ya magari ya Serikali.

Mathias Mbafu

Posts : 6
Join date : 2012-03-09

View user profile

Back to top Go down

MATENGENEZO YA MAGARI CHINI YA UDHAMINI

Post  Rutaihwa on Wed Oct 05, 2011 4:40 pm

NASHUKURU KWA USHAURI HUO.

Nafikiri kwa sasa ni wakati muhafaka kuishauri PPRA kutoa mwongozo huo ili TEMESA wasing'ang'anie magari hayo kama ilivyo kwangu.

Rutaihwa

Posts : 58
Join date : 2011-09-29
Age : 51

View user profile

Back to top Go down

MATENGENEZO YA MAGARI

Post  freddy.mbeyella on Wed Oct 05, 2011 1:21 pm

Ni kweli kanuni hiyo inataka magari ya umma yafanyiwe matengenezo TAMESA. Kwa maoni yangu magari yaliopo katika uangalizi wa muuzaji yanapaswa kufanyika katika karakana za muuzaji tu vinginevyo masharti ya uangalizi yatakuwa yamekiukwa inaweza ikasababisha kupoteza haki za waranti.

Waranti(udhamini) ni ahadi ambayo hutolewa na muuzaji kwa mununuzi wa bidhaa kwamba endapo wakati wa mauzo au baaada ya mauzo kwa kipindi fulani kutakuwa na hitilafu yoyote muuzaji atatengeza au kubadilisha bidhaa bila gharama yoyote. Moja ya masharti huwa ni lazima bidhaa hiyo iwe chini ya uangalizi wa muuzaji. Endapo itadhihilika kuwa bidhaa hiyo imefanyiwa matengenezo nje ya makubaliano dhamana hiyo itakoma.

freddy.mbeyella

Posts : 74
Join date : 2009-08-25

View user profile

Back to top Go down

MATENGENEZO YA MAGARI

Post  Rutaihwa on Thu Sep 29, 2011 5:53 pm

KANUNI NAMBA 59 YA UNUNUZI WA UMMA GN 97 INATAKA MAGARI YATENGENEZWE TEMESA.JE,KWA MAGARI AMBAYO YAKO CHINI YA MKATABA UANGALIZI WA MUUZAJI(WARANTY PERIOD) YANARUHUSIWA KUPELEKWA TEMESA? NISHAURINI ,MWENZENU NINA HII KASHESHE HAPA OFISINI.

Rutaihwa

Posts : 58
Join date : 2011-09-29
Age : 51

View user profile

Back to top Go down

Re: MATENGENEZO YA MAGARI

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum